Makala
MUNGU ANAPOITAKA SHUKRANI YAKO:
| Makala
1 Wathesalonike 5:18
Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Shalom watu wa Mungu!!
Katika kila jambo maishani mwetu kuna kusudi la Mungu. Yapo mambo yanatufurahisha lakini pia yapo ambayo yanatuchefua na kutuvunja mioyo. Lakini yote katika yote tunapaswa kumshukuru Mungu.
Kuna watu tumezoea kumshukuru Mungu pale tunapofikwa na mazuri tuu, lakini tukifikwa na mabaya ni wepesi wa kulaumu na kunung'unika.
Maisha yetu yanatakiwa yawe ya shukrani mbele za Mungu kila iitwapo leo.
Mshukuru Mungu asubuhi, Mshukuru Mungu mchana, Mshukuru Mungu jioni hata usiku.
Kila siku, kila saa umshukuru Bwana!!
Kuna watu wakisikia kumshukuru Mungu wanajua hadi utoe sadaka,,
Sikia Unaweza kumshukuru Mungu kwa kinywa/Mdomo na bado ikawa sadaka tosha kwa Mungu!!
Imeandikwa :""""
Hosea 14:2
2 Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie BWANA; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng’ombe.
Ndani ya Shukrani kuna Baraka za Mungu juu yako kwa ajili ya maisha yajayo kwako!!
Lakini pia Nataka ujue kwamba shetani anaweza kuvuruga moyo wako, kiasi kwamba ndani ya moyo wako huoni haja ya kumshukuru Mungu kabisaa.
Lakini kwa Mungu iko Nguvu inayoweza kukufungua na kukurudishia sauti ya shukrani ndani ya moyo wako!!
Biblia inasema hivi;
Yeremia 33:11
11 BWANA asema hivi itasikilikana tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, na sauti yao wasemao Mshukuruni BWANA wa majeshi, maana BWANA ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa BWANA.
Anaposema itasikilikana tena anamaanisha ilikuwepo ila kuna kitu kimevuruga isiwepo tena. Kama ndani yako kulikuwa hakuna sauti ya kumshukuru Mungu, Ninakuombea Mungu akurudishie kwa Jina la Yesu!
Mshukuru Mungu kila saa, kila dakika, kila sekunde. Mshukuru Mungu kila siku, kila wiki, na Mshukuru Mungu kila mwezi!!
Mungu awabariki Sana Sana!!
Pastor Innocent Mashauri
Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA
Maarifa ya kiMungu
+255 758 708 804
www.sirizabiblia.com
SADAKA